Thursday, 12 September 2013

JOCATE: ACHENI MAJUNGU,TUFANYENI KAZI ILI KUJENGA TAIFA LETU




Msanii wa filamu na pia mwana mitindo maarufu hapa nchini Jocate Mwegelo maarufu ‘Kidoti’ amewataka watu kutokufatilia mahusiano yake na Luciano Gadie Tsere ‘Lucci’.

Jocate amesikitishwa sana na taarifa ambazo amekuwa akizipata tangu atoe wimbo wake wa kaka dada aliyo mshirikisha Lucci.

“Watu wengi wana fatilia maisha yangu yakimapenzi kwasasa nawengine kudai kuwa tunamegana kishkaji,natoka naye ,sitoki naye haiwahusu hata kidogo kwasababu ni maisha yangu,sio kila kinaoonekana kwenye video ya wimbo ni vitu vya kweli

Yale ni maigizo, mimi ni msichana na nastahili kuwa na mpenzi ila tusiharibiane majina kwa maneno machafu”,alisema.

Jocate amefunguka hayo katika page yake ya twitter pamoja na instagram,napia aliwasihi watu kutokudanganyika na uzuri wake nakuwa na imani kuwa kila mtu ambaye yuko nae no mpenzi wake.


No comments:

Post a Comment