Friday 28 February 2014

NYOTA WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA AFRICA MASHARIKI,NASEEB ABDUL MAARUFU DIAMOND PLUTNUM AMEWEKA WAZI KUWA ANAKERWA NA TABIA ZA WASANII WANAOPENDA KUMCHAFULIA JINA WAKATI KILA MTU ANAHANGAIKIA MAISHA YAKE



Diamond alisema kuwa kuna baadhi ya wasanii humpakazia kuwa yeye anawasema wasanii wengine wamuziki wa kizazi kipya hususan kazi zao wakati yeye hajawahi kukaa nakumzungumzia mtu kuhusu muziki anaofanya.

"Kila mtu anahangaikia maisha yake binafsi,tusiiingiliane maisha,mi na hustle kwa staili yangu na kamwe maneno yao hayawezi kunirudisha nyuma",alisema

DOGO ASLAY AELEZA SABABU ZILIPELEKEA YEYE KUNUNUA GITAA NA KINANDA


Dogo Aslay alilieleza papaso la burudani kuwa Vifaa hivyo vitaweza kumsogeza na kuhakikisha kazi zake zinafanyika kiundani zaidi kutokana na nia yake yakuwa msanii bora nasio bora msanii!