Monday, 2 September 2013

Elizabeth Micheal( LULU) : Wasichana wenzangu kuweni makini na Wanaume mmaochagua katika mahusiano



Elizabeth Micheal(  LULU) : Wasichana wenzangu kuweni makini na Wanaume mmaochagua katika mahusiano


Msanii anaitikisa tasnia ya filamu kwasasa hapa nchini,Elizabeth Micheal maarufu ‘Lulu’amewataka mashabiki kutambua kile wanacho kihitaji katika mapenzi.

Mara nyingi wasichana wanakuwa wakionewa katika maisha yakimapenzi kutokana na kuwa hawatambui wanaocho kihitaji katika mapenzi na pia kutokujua haki zao zakimapenzi.

Akizungumza juz katika ‘Pillow Talk’ ya Times Fm lulu aliwasihi mashabiki wa kike kuwa makini na yule anaye mchagua kuwa mpenzi wake na kuto kukubali kupelekeshwa katika mahusiono ili tu wafikie malengo yao.

“Mimi kwanzia sasa baada ya kuwa nimeamua kuwa Lulu mpya nitakuwa makini sana pale ntakapo hitaji tena kuwa na mpenzi,nita hitaji mwanaume atakaenipenda,atakae kuwa kama kaka yangu,baba yangu na kuwa tayali kunielekeza pale anapoona nakosea”,alisema Lulu.




No comments:

Post a Comment