Sunday, 2 June 2013

HUDDAH: NATAKA MWANAUME MWENYE HELA MIMI NI GOLD DIGGER



  Juzi usiku wakati washiriki wa BBA walipokuwa wakifanya zoezi la "speed dating", walielekea eneo la garden na kukuta meza zenye mishumaa, ambapo pembeni ya meza kulikuwa na hearts 7 zikiashiria wasichana wanapotakiwa kukaa, wakati upande wa pili yake kulikuwa na maua rose 7 yakiashiria wanaume wanapotakiwa kukaa.
wakati wa date yake (Huddah) fupi na mshiriki kutoka Uganda (Denzel), Huda alifunguka kuwa anataka mwanaume mwenye pesa na kusema kuwa yeye ni "gold digger", baada ya jamaa kumuuliza maswali mengine juu ya jilo, kwa haraka alibadili tamko lake na kudai kuwa alikua anatania
wakati huo huo, kila mmoja alipata nafasi ya dakika mbili kudate na mwingine

No comments:

Post a Comment