Kamati ya mipango ya mazishi ya marehem Ngwea wametoa taarifa mpya
kwamba mwili wa ndugu yetu Albert Mangwea utafika siku ya juma pili ya
tarehe 2 / 6 saa nane mchana na sio siku ya jumamosi kama
ilivyotaarifiwa hapo awali.
sababu za mwili wa Albert Mangwea kushindwa kufika jumamosi kama
ilivyopangwa ni kutokana na watanzania waishio Africa Kusini, kuomba na
wao kutoa heshima za mwisho
kwa maana hiyo basi taratibu zote za kuaga mwili wa marehemu Albert
Mangwea, kwa wakazi wa Dar es salaam na maeneo ya jirani zitafanyika
siku ya jumatatuya tarehe 3 / 6 kuanzia saa mbili ya asubuhi mpaka saa
sita mchana, ambapo baada ya hapo, safari rasmi ya kuelekea Mororgoro
itaanza kwa ajili ya mazishi itaanza.
kamati inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza
No comments:
Post a Comment