MSANII wa
filamu napia mwanamitindo hapa nchini,Jocate Mwegelo ametoa fursa kwa wote
wanaopenda kuwa wanamitindo hapa nchini kuijiunga katika kundi lake
linalotambulika kwa jina la Kidoti Club.
Kupitia
kundi hili (Club) ambalo limezinduliwa rasmi tarehe 18/12/2013, wadau watapata
nafasi yakupokea dondoo mbalimbali kuhusu urembo,mavazi,na maswala yakijamii
yatakayo wasaidia katika mambo mbalimbali ikiwemo ajira.
“Ajira
kwasasa hapa nchini imekuwa changamoto sana na vijana wengi wanashindwa kujua
wapi pakuanzia kutokana na kuwa hakuna wakuwashika mkono”,alisema Jocate.
Kundi la
Kidoti itawezesha watu mbalimbali kujipatia zawadi muhimu zakuwawezesha kuziba
pengo la baadhi ya mahitaji yao katika maisha yao ya kila siku kupitia kujibu
maswali watakayo kuwa wakiulizwa katika kundi hilo ikiwa ni pamoja na kupata
mawazo tofauti kutoka kwao kama chemsha bongo
“Zawadi ni
nyingi kwakweli na baadhi ya hizo ni Tisheti,vipodozi,nywele (Wig) nakadhalika
na zitatolewa kwa wale wenye uwezo mkubwa wakujibu maswali kutoka Kidoti
Club”,alisema
No comments:
Post a Comment