Baada ya kupotea nchini kwa takribani wiki mbili hatimaye
mwigizaji mwenye mafanikio makubwa sana nchini Vicent Kigosi “ Ray”
Amerejea Tanzania Tokea Dubai na vifaa vipya kabisa na vya kisasa kwa
ajili ya utengenezaji wa filamu chini ya kampuni yake ya RJ company
yenye makao makuu huko sinza Dar es Salaam.
Ray ambaye aliondoka nchini takribani wiki nne zilizopita
amekuja na vifaa ambavyo ye mwenyewe anasema hamna mtu wala mwigizaji
yoyote anayetumia vifaa kama hivyo Afrika mashariki na kati kwa ajili ya
filamu.
“Unajua soko la filamu linakua, kila siku teknolojia inaongezeka
na kuwa kubwa, tukiendelea kulala na kutumia vifaa vyetu vya kizamani
hatufiki popote, ndo maana nimeamua kuja na vitu ambavyo naamini
vitaobgeza ubora wa filamu zetu” Aliongeza Ray alipokuwa akizungumza na
bongomovies.com.
No comments:
Post a Comment