Imefahamika kuwa marehemu Langa Kileo aliye kuwa Rapper kwenye familia
ya bongofleva atazikwa jumatatu juni 17,2013 kwenye makaburi ya
kinondoni jijini Dar es salaam.
Baba mdogo wa marehemu amesema "Dokta wa Muhimbili aliye kuwa ana mtibu
Langa mpaka dakika ya mwisho ametuambia Langa amefariki kutokana na
Malaria ,Alikuwa na Malaria point 7 na mwisho wake ika badilika na
kupanda kichwani.
Mama yake marehemu Langa alikuwa amekwenda Marekani kwa shughuli zake
na anatarajia kurudi muda wowote kutoka sasa alisema Baba mdogo wa
Marehemu Langa Kileo.
No comments:
Post a Comment