Exclusive toka kwa Irene Uwoya! Kama una kipaji cha kuigiza hii inakuhusu...
Mwigizaji mwenye mvuto wa pekee ndani ya bongomovies Irene uwoya
a.k.a mama krisna amewakata wakazi wa Morogoro na Dodoma wenye vipaji
vya kuigiza kukaa mkao wa kula kwani anatafuta waigizaji zaidi ya
thelasini (30) kwa ajili ya kuigiza naye movie yake mpya itakayotoka
mwishoni mwa mwezi wa sita au mwanzoni wa mwezi wa saba. Akizungumza na
mwandishi wetu. Irene uwoya amesema kuwa kutakuwa na usaili kwa ajili ya
kuwapata waigizaji hao na ametaka vikundi vya uigizaji vya kioa
iliyotajwa hapo juu kujiandaa na kujipanga kwani movie yake mpya hii
itakuwa ya kwanza na ya aina yake katika historia ya movie za kibongo.
"watu wamezoea kumuona Irene akigiza ndani ya nyumba nzuri na
magari mazuri kila siku, hawajui kama Irene huyu huyu anaweza kufanya
movie kama mtu wa kijijini sana asiyejua hata matumizi ya simu ni nini"
aliongeza Irene. "Nataka kufanya kitu cha tofauti kabisa mpaka watu washangae kama ni mimi kweli, hii movie itakuwa ya kwanza Tanzania"
Alizidi kusema.
Ndani ya movie hiyo mpya Irene Uwoya amesema atashirikisha
vipaji vipya tuu ambavyo havijawahi kuoneka kwani anaamini bado kuna
vipaji vikubwa sana vimejificha hasa mikoani na anataka kuwapa nafasi
ili waweze kuonesha uwezo wao ndani ya Tasnia hii ya bongomovies.
No comments:
Post a Comment