Ikiwa ni miezi mitatu tu imebaki girlfriend wa Rapper Ney wa mitego
"Siwema" kujifungua, Ney ameongea juu ya kushuka kwa mafanikio ya
wasanii mara baada ya kuoa, ambapo yeye hatarajii kuoa hivi karibuni.
Ney amesema wengi wa wasanii bongo mara tu baada ya kuoa wanashuka
kimziki na kuwataja majina kwa kuwatolea mfano ambapo amesema Marlow
kapotea baada ya kuoa, Matonya, Z Anto na Shetta pia nyimbo zake kadhaa
zimebuma baada ya kuoa.
"kuna ngoma yangu inaitwa "utakula jeuri yako", ambayo inaelezea
vitu vyote hivyo, ambavyo may be watu hawavijui, aaah na pia inaonyesha
unatakiwa kufanya nini ukiwa kwenye mazingira hayo, ya kwamba tayari
umeshakuwa kwenye ndoa, wasanii wengi sana sio tanzania tu dunia nzima,
ukioa au ukiolewa na game yako inaisha, otherwise unatakiwa kuwa mjanja
sana, kama alivyokuwa mjanja Jay Z na Beyonce, zipo techniques ambazo
unatakiwa kufanya, sio kukurupuka tu na kuoa, na ndio maana asilimia
kubwa hasa kibongo bongo sisi wengi ambao wameoa wamefeli , kwa
aslilimia nyingi sana wamefeli ijapokuwa hili tatizo ni la dunia
nzima."
"wapo wengi ndugu yangu Matonya alipotea, Z Anto alivyooa kapotea,
Marlow alivyooa kapotea, Shetta kaoa juzi tu zimebuma kadhaa hapa
katikati, nafikiri hii ni mifano hai ambayo ipo, so watu wanatakiwa
kujipanga, so ukiskia mi nimeoa ujue nimejipanga, najua hatua mia
zitakuja mbele, cause i know what am doing, hao waliooa wana nyimbo
nyingi nzuri na zinatoka lakini zinakuwa hazikiki kama mwanzo
walivyokuwa wakitoa nyimbo, sio kwamba wanakuwa hawarikodi wanarikodi ,
wimbo mzuri, na kiwango chako kinaweza kuwa hakijashuka, lakini mapokeo
yanakuwa ni tofauti, na sio msanii tu hata wafanya biashara na
watangazaji pia
No comments:
Post a Comment